Mwanaye aliyekuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi
wa al Qaeda Osama bin Laden, ameapa kulipiza
kisasi kwa mauaji ya babake.
Katika ujumbe wa sauti uliochapishwa katika
mitandao Hamza bin Laden ameapa kulipiza kisasi
kwa Marekani kwa kumuua babake 2011 huko
Pakistan.
Ujumbe huo wa dakika 21 wenye kichwa "We Are All
Osama,", Hamza ambaye inaaminika kuwa alikuwa
na babake makomando wa Marekani walipowavamia
na kumtwaa ameapa kuendeleza kazi aliyoianza
babake.
''Tutaendelea kuwasaka na kuwapiga popote pale
mtakapokuwa mumejificha ati nyuma ya pazia za
usalama kwa maovu munayoyaendeleza ,Palestina,
Afghanistan, Syria, Iraq, Yemen, Somalia na kote
kwenye ardhi ya waislamu mnayokalia '' shirika la
habari la Reuters linamnukuu.
''na kwa wale wanaodhania kuwa tutakuwa
tukilipiza kisasi mauaji ya Osma ole wenu, kwanini
sisi tutakuwa tukilinda dinia ya kiislamu'' alisema
Hamza.
Osama aliuawa na makomando wa marekani katika
maficho yake huko Pakistan mwaka wa 2011.
Hamza ambaye kwa sasa ana umri wa kati ya miaka
ishirini hivi alikuwa na babake kabla ya
mashambulizi ya kigaidi ya mwaka wa 9/2001 huko
Afghanistan kabla ya kukimbilia Pakistan kufuatia
mashambulizi makali ya Marekani na washirika
wake.
Hamza kulingana na wachanganuzi anatambulishwa
na kiongozi wa kidini wa kundi hilo Ayman al-
Zawahiri katika ujumbe huo unaolenga kuwavutia
vijana ambao kwa sasa wamejiunga kwa wingi na
kundi la Islamic state.
Source (bbc swahili)






Post a Comment