Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Timu ya Mwadui FC, imepata pigo kubwa baada
ya kukimbiwa na wachezaji wake muhimu wa
kikosi cha kwanza na wenye uzoefu mkubwa na
Ligi ya Vodacom.


Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’
ameiambia Goal, hali hiyo haitakiteteresha
kikosi chake na kusema anawaamini chipukizi
waliopo wataweza kutimiza malengo ya timu
hiyo msimu ujao kwa kubeba taji la ligi ya
Vodacom.



“Nikweli wameondoka baada ya kumaliza
mikataba yao na msimu ujao nitakuwa na kikosi
ambacho kina majina mapya siyo julikana lakini
nitawapa nafasi kwa sababu wana uwezo
mkubwa na ndio watakaotupa ubingwa kama
ilivyokuwa kwa Leicester kwenye ligi ya
Uingereza msimu uliopita,” amesema Julio.


Wachezaji walioondoka na kwa sasa wanasaka
timu za kuzitumikia msimu ujao ni Nizar
Khalfan na Razak Khalfan, Jeryson Tegete,
Jabir Aziz, Athuman Idd, Rashid Mandawa,
Malika ndeule na Jamali Mnyate.

Thanks For Visiting, Our Website Come Again For News, Advertisement And Good Articles

Keep This blog site In Your Mobile For More Updates

Facebook Blogger Plugin by Tanzaniastar
https://www.facebook.com/Tanzaniastar

Post a Comment

 
Top