Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

ANTHONY MARTIAL AITOSA MANCHESTER
UNITED TWITTER



Anthony Martial ameitosa Manchester United
kutoka kwenye kurasa za twitter alizokuwa
akizifuata baada ya kubadilishiwa namba ya
fulana yake.

Nyota huyo wa miaka 20 aliyetua Old Trafford
msimu uliopita wa majira ya joto, ameipoteza
namba yake pendwa ya fulana badala yake
amepewa jezi namba 11 kwa msimu ujao ili
kumpisha Zlatan Ibrahimovic.

Martial alizua tetesi za kutokuwa na furaha
kwa mabadiliko hayo Jumamosi kwa kutupia
picha kwenye ukurasa wake wa Facebook
ikimwonesha akiwa ndani ya jezi ya namba tisa
baada ya kufunga goli katika mechi ya nusu
fainali Kombe la FA dhidi ya Everton.


Sasa Mfaransa huyo ameamua kwenda mbali
zaidi kwa kuiondoa klabu hiyo kwenye ukurasa
wake wa Twitter na Instagram Jumapili
asubuhi.

Martial si sehemu ya kikosi cha United kilichopo
ziarani China kwani anaendelea kufurahia likizo
yake baada ya fainali za Euro 2016
zilizofanyika Ufaransa.

Souce (goal.com)

Thanks For Visiting, Our Website Come Again For News, Advertisement And Good Articles

Keep This blog site In Your Mobile For More Updates

Facebook Blogger Plugin by Tanzaniastar
https://www.facebook.com/Tanzaniastar

Post a Comment

 
Top